ATHARI ZA MINYOO KWA KUKU
Minyoo
kwa kuku ina athari nyingi, athari ambazo zinaweza hadi kumpatia hasara
mfugaji kama hatozingati ratiba ya kuwapa dawa ya minyoo kuku wake kila
baada ya miezi mitatu. Athari za minyoo kwa kuku ni kama zifuatazo:-
Minyoo
mara zote ndani ya mwili wa kuku hutumi virutubisho ambavyo tayari
vishameng'enywa na kuku, hali ambayo humfanya kuku kushindwa kurudisha
au kufidia nguvu (digestible energy) aliyoipoteza katika kumeng'enya
chakula, atashindwa pia kupata virutubisho vya ukuaji (nutrients for
growth) , na kama haitoshi pia atakosa kupata virutubisho vya uzalishaji
(nutrients for production), hali ambayo itamfanya kuku kudhoofika,
kudumaa, kupunguza au kutotaga kabisa na hatimaye kufa.
No comments:
Post a Comment