Thursday, April 10, 2014

UGONJWA WA KUHARA DAMU KWA KUKU (COCCIDIOSIS)

        Coccidiosis ni ugonjwa wa kuhara damu unaosababishwa na vijidudu wajulikanao kwa jina la "Protozoa". Wadudu hawa hushambulia sehemu mbalimbali za utumbo wa kuku.


Mazingira yanayosababisha coccidiosis. 
  • Unyevu kwenye matandazo/maranda (litter material). 




  • Kutobadilisha matandazo/maranda kwa muda mrefu.

  • Kuhamishia vifaranga kwenye sehemu waliyokuwa wanakaa kuku wakubwa bila kufanya usafi.


Dalili za coccidiosis.
  • Kuharisha; kwanza kinyesi huanza kuwa laini, pili hubadilika rangi kuwa kijivu na baadaye mchanganyiko wa damu na kuonekana kama kahawia au rangi ya udongo au brauni.
 
                                                              
  • Manyoya yasiyo na mpangilio na yaliyosinyaa, kuku hapendezi na hukunja mabawa kama amevaa koti.

  • Kuku kupauka(paleness), hususani kwenye viremba(comb/wattle) na miguuni kutokana na kukosa damu.

  •  Kukua polepole(poor growth).

  •  Kukosa hamu ya kula.

  • Vifo vingi hasa vifaranga.
  • Kupungua uzito.

  • Kushusha utagaji.


 Namna ya kuzuia coccidiosis.
   1.  Epuka unyevu kwenye maranda(litter material) na banda kwa ujumla.  

   2. Tumia dawa za kukinga ugonjwa (coccidiostats).

   3. Badilisha maranda kabla ya kuingiza vifaranga au kuku wapya.


 Jinsi ya kutibu coccidiosis.
Tumia (i)  Esb3 - Kwenye maji au 
           (ii) Amprolium -Kwenye maji. 


MUHIMU
''''''Matibabu yote ni muhimu kutumia dawa ya vitamin (multivitamin) kama nyongeza kwa muda wa siku tatu zinazoachana kwa ajili ya kuongeza hamu ya kula''''''








Usikose kufuatilia mfululizo wa mada zetu............................!!!











Imeandaliwa na; 

Dr. Lihundu A. A.
+255 766 828344








No comments:

Post a Comment