NIJIBU DOKTA

6 comments:

  1. Habari dokta, mi ni mfugaji mpya wa kuku wa mayai,wamefikisha wiki 36 sasa, ila kuku wangu wanadonoana sana hadi kufikia kupeana majeraha. Nifanyeje?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole sana kwa tatizo la kuku wako. Kinachotakiwa kufanya ni kuwakata midomo kwanza kama bado haujawakata, kisha waboreshee chakula kwa kuwaongezea madini ya calcium. Ahsante kwa kutembelea blog yetu.

      Delete
  2. Habari yako Dk.

    Niliwahi kusoma kwenye gazeti moja kuwa kuku Broila ni hatari kwa afya ya binadamu, lakini bado watu wanawatumia.

    Madhara yake huanza kujitokeza baada ya muda gani?

    ReplyDelete
  3. Habar ni nzur mpendwa, kuku wa nyama ambao ni broilers hawana madhara yoyote kwa afya ya binadam, ispokuwa binadam wenyewe ambao ni wafugaji wanafanya uchakachuaji ambao unapelekea baadhi ya kuku kuwa na madhara.
    Hapa namaanisha kwamba kuna baadhi ya wafugaji wanaongeza viambata katika chakula cha kuku ambavyo vinamadhara kwa afya ya mwanadam, na hii inatokana na haraka ya kupata faida.
    Ahsante kwa kuuliza na karibu kwa maswali zaidi.

    ReplyDelete
  4. Heshima yako Dk.

    Nafurahia masomo yenu mnayoyatoa hasa siku zile ulipokuja kunitembelea na kunishauri namna bora ya kufuga kuku. Na nimekitumia chakula chenu, ni kizuri sana.

    Nina swali naomba msaada wako Dk.
    Kuku wangu ninatarajia kuwachanja gumboro tarehe 3/8/2014, je, ni wakati mzuri kuwapa chanjo hiyo? Yaani ni asubuhi, mchana ama jioni?

    Natanguliza shukrani.

    ReplyDelete
  5. Nafurahi kufaham unafurahia masomo yetu.
    Kuku unaweza kuwapa chanjo wakati wowote, cha kuzingatia ni kuwanyima maji kwa muda ili wapate kiu na kuweza kunywa maji yenye chanjo kwa ufanisi.
    Ahsante kwa kuuliza na karibu tena kwa maswali zaidi.

    ReplyDelete