FAIDA ZA UFUGAJI KUKU
Tunafaham kuwa unajua faida za kuku lakini ngoja tukumbushe yafuatayo kuhusu faida za ufugaji kuku.- Kuku ni chanzo cha haraka cha pesa kwa kuuza kuku au mayai.
- Kuku wanaweza kabisa kukuongezea kipato na kukuondolea kabisa umaskini.
- Nyama ya kuku na mayai ni protini muhimu kwa familia, yaan watoto, wagonjwa na hata wazee.
- Kinyesi cha kuku pia ni mbolea, lakini kama haitoshi maganda ya mayai na manyoya ni mapambo.
- Hakuna dini wala utamaduni wowote Tanzania unaozuia kula kuku.
- Katika nyama ambayo haina madhara yoyote katika mwili wa binadamu ni nyama ya kuku na samaki.
- Ni mradi unaompa fursa kusimamia hata mwajiriwa bila kuathiri ajira yake.
- Na kwa wale akina fulani katika shughuli za kijadi kuku ni moja ya zawadi au malipo kama mteja hana pesa.
No comments:
Post a Comment