Thursday, March 27, 2014

UJENZI WA BANDA BORA LA KUKU

Mfugaji anaweza kudhani kuwa mradi wa kuku unaweza kumpatia faida kubwa bila kujali uwepo wa banda zuri na imara.

Banda lililojengwa imara hudhibiti maadui wa kuku na kufanya uzalishaji kuwa bora zaidi.

Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa ujenzi wa banda:
 1. Idadi ya kuku
            Kabla ya kuanza kujenga banda, mfugaji anatakiwa kujua kuwa anataka kufuga kuku wa aina
         gani na wangapi. Hii itamwezesha mfugaji kujua ukubwa wa banda linalohitajika.


     2. Uwezo wa Mfugaji Kifedha.
            Ujenzi wa banda unahitaji fedha nyingi hivyo ni lazima mfugaji ajue kuwa banda analotaka
         kujenga atalimaliza.

     3. Eneo la kujenga banda.
            Mfugaji lazima awe na eneo la kujenga banda na liwe na sifa zifuatazo:-
 • Mwinuko - Iwe sehemu iliyoinuka isiyotuamisha maji kirahisi.
 • Eneo lisiwe mbali na sehemu ya kuishi ili kuweza kulinda.
 • Uwezekano wa Upanuzi - Sehemu iwe pana na kubwa ili mradi ukiwa mkubwa iwepo sehemu ya upanuzi.
SIFA ZA BANDA BORA LA KUKU.
 1. Liwe limejengwa..... mahali palipokingwa na upepo mkali kwa miti.
 2. Liwe na mwanga wa kutosha.
 3. Madirisha yaruhusu hewa safi kuingia na chafu kutoka (Cross Ventilation).
 4. Sakafu isiruhusu maji kutuama wala maeneo yanayozunguka banda.
 5. Paa lisiruhusu mvua kuingia.
 6. Banda liwe linasafishika kwa urahisi.
 7. Kuta ziwe imara na zizuie wanyama waharibifu kuingia.
 8. Banda liwe na nafasi ya kutosha kwa ajili ya kuku, vyombo vya maji na chakula na mhudumu kupita.

Usikose muendelezo wa darasa letu.

Imeandaliwa na;

Dr. Lihundu A.A.
+255766828344


No comments:

Post a Comment