SIFA ZA JOGOO NA TETEA BORA
1. SIFA ZA JOGOO BORA
- Awe na umbo kubwa
- Awe na ukiko nzuri usioangukia upande mmoja
- Awe mchangamfu
- Apende kuwa na himaya yake. Sifa hii utaigundua pindi ukimjazia wapinzani, atakuwa anapigana badala ya kufuata matetea.
2. SIFA ZA TETEA BORA
- Awe na umbo kubwa
- Awe na uwezo wa kuatamia
- Awe na uwezo wa kulea vizuri (high mothering ability)
- Aweze kutaga mayai ya kutosha.
ATHARI ZA KIMAZINGIRA KATIKA ULAJI WA KUKU
Kuna sababu
mbalimbali zinazoathiri ulaji wa kuku, athari hizo zinaweza zikamfanya
kuku ale sana au asile kabisa. Zifuatazo ni sababu za kimazingira
zinazoathiri ulaji wa kuku:-
1. JOTO
Ulaji
wa chakula hupungua kadri joto la mazingira linavyoongezeka, kwan kama
tujuavyo zoezi la umeng'enyaji wa chakula huongeza joto la mwili, na
joto la mwili halitakiwi kupanda wala kupungua, hivyo basi ubongo
unamuamuru kuku asile ili kudhibiti joto la mwili lisipande.
Angalizo ni kwamba mfugaji anatakiwa achunge hali ya joto la banda, kwan
hata akizidisha balbu au banda likikosa hewa ya kutosha pia inaweza
kusababisha joto la mazingira kuongezeka na kupelekea kuku kukosa hamu
ya kula hali amabayo itawafanya kuku wadumae.
2. BARIDI
Kipindi cha baridi kuku wanakula sana kwa
sababu ubongo unamuamuru kuku ale sana kwa kuwa umeng'enyaji unatakiwa
uwe mara kwa mara ili kudhibiti joto la mwili lisishuke.
3. MHEMUKO (STRESS)
Banda
likiwa chafu, au lipo sehemu yenye kelele za mara kwa mara, au umeweka
kuku wengi katika banda dogo itawasababishia kuku kupata stress hali
ambayo itawafanya kuku wakose hamu ya kula.
4. UPATIKANAJI WA MAJI
Maji
yanakazi kubwa sana katika umeng'enywaji wa chakula (digestion
process), kwa hiyo kuku ukiwabania maji na ulaji wao pia utapungua,
kwani zoezi la umeng'enyaji chakula utakuwa unafanyika taratibu sana
hali ambayo itawafanya kuku kukaa muda mrefu bila kuhitaji chakula.
5. MUUNDO WA VYOMBO VYA CHAKULA NA MAJI
Muundo
mbovu wa vyombo vya chakula na maji utasababisha chakula au maji
kuchanganyika na vitu visivyofaa (feed or water contamination) kama vile
kinyesi hali ambayo itapunguza ulaji wa kuku.